Shirika la Ndege la Discover kutoka nchini Ujerumani limeongeza safari zake kutoka safari mbili kwa wiki walizokuwa wakifanya hapo awali na kufikia safari nne kwa wiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wa Zanzibar (AAKIA).

Shirika hilo la Ndege lilikuwa na ratiba ya kuwasili Uwanjani hapo siku za Jumanne na Ijumaa tu kutoka Ujerumani kupitia Mombasa na kuishia Zanzibar ambapo kwa sasa limeongeza siku ya Alhamis na Jumamosi kuwa safari za moja kwa moja (DIRECT FLIGHT) kutoka Frankurt hadi Zanzibar.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) ndio Uwanja unaoongoza kwa safari nyingi zaidi za Ndege Afrika Mashariki kwa kuwa na zaidi ya safari 62,393 kwa Mwaka.