Ndege ya Shirika la Air France ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) Jumatatu ya tarehe 26 Mei 2025 majira ya saa 2:57 usiku ikiwa na abiria 158 kutoka nchi Ufaransa.
Ndege ya Air France imerejesha safari zake katika Uwanja huo wa Ndege baada ya mara ya mwisho kutua mwezi Machi 2025 kutoka na msimu mdogo wa abiria (low season).
Safari za Ndege ya Shirika hilo za moja kwa moja (direct flight) zitakuwa zikifanyika mara tatu kwa wiki ambazo ni Jumatano, Alhamis na Jumamosi.