
KARIBU TENA ZANZIBAR, ETIHAD AIRWAYS.
Jumapili ya tarehe 14 Juni 2026, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA)umepokea safari ya kwanza ya kurejea kwa Shirika la Ndege la Etihad kutoka Abu Dhabi.
Ndege ya Airbus A320-EY791,imetua majira ya saa 7:13 mchana ikiwa imebeba abiria 152.
Etihad Airways imerejesha safari zake katika Uwanja wa Ndege wa AAKIA baada ya kusitisha kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili ambapo sasa itakuwa ikifanya safari nne kwa wiki kati ya Abu Dhabi na Zanzibar katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili, hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za utalii, biashara na uwekezaji kwa Zanzibar.
#AAKIA #ZanzibarAirportsAuthority #EtihadAirways #DestinationZanzibar #Aviation Tourism




