ZAA Kinara Michuano ya Mei Mosi Unguja 2026.

Wana anga wa klabu ya Mpira wa Miguu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar jana Jumatatu ya tarehe 27 April 2026 wameibuka kidedea baada ya kuwachakaza wachimba chumvi wa Shirika la Bandari Zanzibar kwa mikwaju ya penanti 5-4 na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa upande wa Unguja.

Mabingwa wa upande wa Unguja watacheza na Mabingwa wa upande wa Pemba katika fainali itakayoamua Bingwa wa Mashindano ya Mei Mosi Zanzibar. Fainali iyo itachezwa tarehe 30 April 2026 katika viwanja vya Maisara saa 10:00 Jioni.