ZIARA YA KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO NA UCHUKUZI

Leo Ijumaa ya tarehe 30 April 2021,Katibu Mkuu Wizara ya UjenzI Mawasiliano na Uchukuzi ndungu Amour Hamil Bakari amekutana na viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar(ZAA) Katika kikao kilichofanyika makao makuu ya ZAA- Kisauni Zanzibar. Kikao hicho pamoja na agenda muhimu za kiutendaji kimelenga zaidi kujitambulisha rasmi kwa katibu mkuu kwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wa ngazi zote wa Mamlaka hiyo.
Copyright © 1953 - 2021 All rights reserved | by Zanzibar Airports Authority (ZAA)
×