DR MWINYI ATEMBELEA TB3 AAKIA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe:Dr. Hussein Ali Mwinyi leo asubuhi ya Jumatano ya tarehe 14 Aprili 2021 amefanya ziara katika jengo jipya la abiria (TB3) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) Akiambatana na mwenyeji wake Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe: Rahma Kassim Ali, Mhe: Rais ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa hivi sasa katika kuelekea kukamilika rasmi ujenzi wa jengo hilo mapema mwezi Mei mwaka huu Hata hivyo ameitaka Wizara pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kushughulikia eneo la nje la jengo hilo pamoja na bustani (landscape) kwa kuwa lina umuhimu sawa na jengo husika Mhe Rais ameagiza kuongezwa kwa idadi ya vizimba (booth) zinazotoa visa kwa wageni mara tu wanapowasili ili kuondoa msongamano wa abiria watakaohitaji huduma hiyo Kadhalika ameagiza kuwekwa kwa mabango yanayoonyesha ratiba za Ndege kwa abiria (flight information display systems) ili kwenda sambamba na huduma bora za viwanja vyengine duniani Katika ziara hiyo, Dr Mwinyi ameahidi kurudi tena kutembelea jengo hilo kabla ya ufunguzi rasmi na kusisitiza utoaji wa huduma za kisasa zinazoendana na hadhi ya jengo hilo kwa sasa Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na eneo la kuwasili abiria, eneo la kuondokea abiria, eneo la wageni mashuhuri (VIP), mikanda ya kubebea mizigo ya abiria (BHS) pamoja na kaunta za kuchekia abiria wanaosafiri (check in counter )
Copyright © 1953 - 2021 All rights reserved | by Zanzibar Airports Authority (ZAA)
×